matangazo

matangazo

Sunday, January 11, 2009

miaka 45 ya mapinduzi ya zanzibar







Leo ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar ambapo Watanzania wote wanaungana katika kumbukumbu ya uhuru wa visiwa vya Unguja na Pemba kutoka kwa utawala wa Sultan wa Oman mwaka 1964.
Sherehe za Mapinduzi mwaka huu zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba ambako Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Amani Abeid Karume anatarajia kuongoza sherehe hizo.
Viongozi mbalimbali wa Zanzibar na Muungano wanatarajiwa kuhudhuria na kutoa hotuba za kuenzi mapinduzi hayo ambayo yaliongozwa na Rais wa kwanza wa Zanzibar, hayati Abeid Amaan Karume. Kama ilivyo ada, mbali ya hotuba mbalimbali, sherehe hizo zitapambwa na burudani mbalimbali zikiwamo ngoma za utamaduni kutoka Visiwani na Bara.
Rais Karume pia anatarajiwa kutangaza msamaha kwa wafungwa kwa mujibu wa mamlaka aliyopewa na Katiba ya Zanzibar kifungu cha 59. Katika sherehe za mwaka jana, wafungwa 25 walisamehewa. Baada ya Mapinduzi hayo ya Januari 12, 1964, Aprili 26, mwaka huo, Zanzibar iliungana na Tanganyika na kuzaa Taifa moja la Tanzania ambalo Rais wa wake wa kwanza alikuwa Julius Nyerere

No comments: