matangazo

matangazo

Thursday, August 5, 2010

MWENGE UKIWASILI



Mwenge wa uhuru ukiwa mpakani mwa Njombe na Ludewa kabla ya kuanza kukimbizwa wilayani Njombe. hao ni baadhi ya wakimbiza mwenge kitaifa waliongozwa na Nassoro Ally Matuzya.Kazi zilizofanywa na mwenge wa uhuru mwaka 2010 wilayani Njombe ni kuweka jiwe la msingi ukumbi wa shule ya msingi Senga, Kukagua hifadhi ya msitu Isalilo,Kufungua zahanati Nundu na kukagua miche ya chai,kukagua ofisi za idara ya maji halmashauri ya Mji Njombe. mbali na hayo pia kufungua tanki la maji na barabara ya chai(Itombololo), kufungua jengo la utawala shule ya sekondari Wanike, kukagua chuo cha ufundi Igwachanya RC na kufungua soka la Igwachanya na baadae mwenge ulikabidhiwa kijiji cha Ludodolelo kilicho mpakani mwa Njombe na Makete tayari kwa kukimbizwa wilaya ya Makete.

No comments: